Baraza la Ukunga na Uuguzi Tanzania (TNMC) limeisimamisha kwa miezi mitatu leseni ya Muuguzi aliyemchoma sindano ya usingizi na kisha kumbaka kuanzia saa nne usiku hadi saa nane msichana mwenye umri wa miaka 16

Damian Mgaya(41) aliyetoroka anadaiwa kumfanyia hivyo msichana huyo aliyekuwa akimuuguza mama yake katika hospitali ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora
Inaelezwa kuwa mara baada ya kumaliza kumbaka binti huyo aliamua kumtupa eneo la kufulia nguo kwenye nyasi akiwa hajitambui na kummwagia maji mwili mzima
Inaelezwa kuwa mnamo mwaka 2017, Damiani akiwa katika kituo cha Afya cha Igurubi, aliwahi kufanya tukio kama hilo, ambapo alipelekwa Polisi na kisha Mahakamani na aliachiwa huru na kurejeshwa kazini mwaka 2018
Taarifa hiyo imetolewa na Msajili wa Baraza hilo, Agnes Mtawa na kusema kuwa baada ya mtumishi huyo kurejeshwa kazini, alihamishwa kutoka kituo cha Afya cha Igurubi na kupelekwa katika hospitali ya Wilaya ya Igunga
Kufuatia mtiririko wa matukio hayo, Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, (TNMC) limeamua kumchukulia hatua ya kusimamisha leseni yake ya kutoa huduma za ukunga na uuguzi popote nchini Tanzania kwa muda wa miezi mitatu
Advertisements