Ofisa wa benki ya CRDB tawi la Ubungo,Andrew Babu(27)na wenzake watatu ambao ni Wafanyabiashara wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,jijini Dar wakikabiliwa tuhuma za Uhujumu Uchumi ikiwamo kula njama,kugushi tembo kadi, wizi na kutakatisha zaidi ya Mil 100.

Mbali na Babu, washitakiwa wengine ni William Sige, Justina Boniphas na Ally Tatupa ambao wote wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 101/2019.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon aliwasomea mashtaka yao Alhamisi Septemba 26, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Agustina Mbando.


Hakimu Mmbando ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 10, 2019 itakapotajwa tena.

Washtakiwa wote walirudishwa rumande kutokana na shtaka la utakatishaji fedha kutokuwa na dhamana.