Nelson Mabeyo, mtoto wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania (CDF), Jenerali Venance Mabeyo ni miongoni mwa watu wawili waliofariki katika ajali ya ndege ya Kampuni ya Auric iliyotokea leo asubuhi Jumatatu Septemba 23, 2019.

Nelson ndio alikuwa rubani wa ndege hiyo iliyoanguka katika uwanja mdogo wa ndege wa Seronera uliopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania.

Ndege hiyo ilianguka asubuhi wakati ikipaa katika uwanja huo kwenda mkoani Arusha.