Mkazi wa Buguruni, Thomas Mgoli (37) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi ikiwemo kujifanya Afisa Usalama wa Taifa anayetaka kumsaidia aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Kelvin Mhina na wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi akisaidiana na wakili wa serikali mwandamizi Wankyo Simon, amedai kuwa, katika shtaka la kwanza imedaiwa, katika tarehe tofauti kati ya Desemba 1, 2017 na Agosti 2019 katika eneo la Mahabusu ya Keko, huko Temeke, mshtakiwa alijifanya kama Mtumishi wa Umma aliyeajiriwa kitengo cha Usalama wa Taifa (TISS)
Katika shtaka la pili imedaiwa kuwa, kati ya Agusti 17 na 29,2019 katika maeneo tofauti ndani ya jiji la Dare es Salaam, mshtakiwa kwa njia ya kudangaya alijipatia Sh. 280,500 kutoka kwa Lucy Ngongoseki kupitia namba mbili za simu tofauti za mtandao wa Airtel akijifanya kuwa yeye Afisa Usalama kutoka TISS anayetaka kusaidia kesi namba 213/2017 ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Jamal Malinzi katika mahakama ya Kisutu kwa ajili
Aidha katika kosa la mwisho imedaiwa, siku na mahali hapo, mshtakiwa alijipatia fedha kiasi cha sh 280,500 huku akijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu
Hata hivyo, baada ya kusomewa mashitaka hayo, Hakimu Mhina alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kumpatia mshitakiwa dhamana, pia haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi hivyo mshtakiwa atakwenda rumande.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 4, 2019.