Rais Donald Trump wa Marekani ametangaza vikwazo vipya dhidi ya Iran baada ya yale mashambulizi katika visima vya mafuta vya Saudi Arabia.

Trump ameeleza kuwa amemshauri Waziri wa Fedha wa Marekani Steven Mnuchin kuvifanya vikwazo hivyo kuwa vikali zaidi.
Kufikia sasa haijabainika wazi ni kipi kitakachofuata. Rais huyo wa Marekani alikuwa amedokeza kwamba kuna uwezekano wa kujibu shambulizi hilo kijeshi.
Kwa sasa bado pande zinazozozana hazijabaini hasa aliyehusika na mashambulizi hayo katika visima hivyo vya mafuta vya Saudi Arabia.
Waasi wa Houthi huko wanadai walihusika na mashambulizi hayo ingawa Marekani inailaumu Iran.