Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma limefanikiwa kuwaua majambazi 12 katika majibizano ya risasi baina ya majambazi hao na Polisi usiku wa kuamkia jana katika eneo la mashamba ya kilemba kijiji cha Kalemba Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma.

Akizungumzia kijijini hapo jana Ijumaa Septemba 13, 2019 Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, Martin Otieno amesema siku za hivi karibuni kumeibuka matukio ya utekaji magari, baadhi ya waliokamatwa walieleza matukio hayo.
Amesema polisi walifika eneo hilo na kuanza kurushiana risasi na watu hao na kuwaua 12 waliokutwa na bunduki tatu aina ya AK 47, risasi 107, mapanga, visu na mabomu matatu ya kurusha kwa mkono.

Advertisements