Spika wa Bunge Job Ndugai, amewapongeza wabunge watatu wa CCM, Mh. Nape Nnauye, January Makamba na William Ngeleja kwa kitendo cha kiungwana cha kumwomba msamaha Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Mh. Job Ndugai amesema Bungeni, leo September 12, 2019, kuwa ni vyema viongozi wote wakafuata nyayo hizo kwa wale wote ambao wamekuwa wakiwakosea hata kama ni wadogo kwako kicheo, kwakuwa uungwana ni vitendo.
Amesema anashangaa kuona magazeti mengi yamekuwa yakishabikia, na kuwachora wabunge picha za ajabu ajabu pamoja na kuandika habari za kishabiki baadhi ya vingozi nchini.
Pia amemshukuru Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwasemehe wabunge hao kwakuwa ni jambo la kiungwana sana kufanya kama binadamu.
Advertisements