Bilionea Jack Ma amestaafu kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Alibaba, baada ya kuongoza kwa miaka 20, akishuhudia Kampuni ya Alibaba ikikua na kuanzisha biashara mpya. Jack amemteua Daniel Zhang kuongoza makampuni hayo.

Katika barua yake aliyotoa kwa umma Septemba, 10, mwaka jana, bilionea huyo ambaye pia ni mwanzilishi wa kampuni hiyo kubwa ya biashara ya mtandaoni alisema Alibaba kamwe haimilikiwi naye peke yake, lakini atakuwa nayo daima.