Mkazi wa kijiji cha Iponya katika Halmashauri ya Mji wa Kahama, Paschal Clement (32), amemuua mkewe Ashura Paschal (30) kwa kumnyonga shingo kisha kujiua kwa kunywa sumu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Richard Abwao, alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa moja jioni katika kijiji cha Iponya.
Alisema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi na kwamba kabla ya tukio hilo, wanandoa hao walikuwa na ugomvi huku mume akimtuhumu mkewe kuwa si mwaminifu kwenye ndoa.
Abwao alisema Paschal baada ya kutekeleza mauaji hayo, alijiiua kwa kunywa sumu ambayo mpaka sasa bado haijafahamika ni ya aina gani na kukutwa chumbani kwake akiwa amelala sakafuni.