JESHI la Polisi Mkoa wa Iringa linamshikilia na kumhoji mwanamke Kabula Masunga(41), anayedaiwa kufanya ushirikiana baada yakukutwa kwenye paa la nyumba ya Mchungaji Jeremia Charles saa 11 alfajiri.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Juma Bwire amesema leo Agosti 20,2019 kuwa mwanamke huyo anatuhumiwa kufanya ushirikina huo eneo la Isele Ilula wilayani Kilolo mkoani Iringa na kusababisha taharuki kwa wakazi wa maeneo hayo.
Amefafanua mwanamke huyo ambaye ni mpagani na mkazi wa Morogoro alikutwa akiwa katika mazingira hayo akiwa amejifunga mavazi ya rangi nyekundu na nyeusi lakini kifua aliacha wazi.
“Pia alikutwa akiwa na ungo uliyofungwa kitambaa ya rangi nyeusi na nyekundu.Amekutwa pia na pembe la ng’ombe na alijifunga hirizi mikononi. Mwanamke huyo alikuwa na wenzake wanne inaodaiwa alikuwa anasafiri nao kwa kutumia ungo,”amesema .
Kamanda Bwire amesema kwa sasa wanaendelea kumhoji zaidi ili kufahamu lengo la kufanya ushirikina huo.