Jeshi la Polisi Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora limewakamata Watu watatu na kuwafikisha Mahakama ya Wilaya ya Igunga kwa tuhuma za mauaji ya Mama wa miaka 55, Veronica Makumbi, baada ya kumtuhumu kuwa ni Mchawi

Watuhumiwa hao wanadaiwa kumuua mwanamke huyo July 28 mwaka huu saa 6:30 usiku.

Waliokamatwa ni Sung’hwa Ngasa, Willson Sunhnwa na Sunhwa Zumbi wakazi wa kitangili.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Elimajid Kweyamba, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Igunga, Lydia Ilunda, alidai washtakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 196 kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2002.

Kesi imeahirishwa hadi Agosti 29, itakapotajwa tena na washtakiwa walipelekwa mahabusu na hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo..