Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Kigoma imemuhukumu miaka 30 jela mkazi wa kata ya Mwanga manispaa ya Kigoma Ujiji, Isack Balayabala (25) baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya Sekondari Kaulananga.
Akisoma hukumu hiyo jana Ijumaa Agosti 16, 2019 hakimu wa mahakama hiyo, Eliya Baha alisema mshtakiwa alitenda kosa hilo Desemba 2018 kwa kumpa ujauzito mwanafunzi huyo.
Katika kesi hiyo ya jinai namba 46 ya mwaka 2019 mahakama hiyo imesema imeridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na hivyo kwa kuzingatia kifungu cha sheria cha 60A kifungu kidogo cha (3) cha sheria ya elimu namba 353 ya mwaka 2002 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016, mtuhumiwa atatumikia kifungo cha miaka 30 Jela
Advertisements