Majeruhi wengine wanne katika ajali ya moto iliyotokea Morogoro, Agosti 10, 2019 wamefariki Dunia, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, na kufanya idadi ya waliofariki mpaka sasa kwenye ajali hiyo kufikia 93.

Vifo hivyo vinafanya idadi ya wagonjwa waliobaki kuwa 21 kati ya 46 waliokuwa wamefikishwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu.

Akizungumza baada ya kutembelea wagonjwa hao leo Ijumaa Agosti 16, 2019, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema madaktari wanafanya kila jitihada kuokoa maisha ya wagonjwa waliobaki.