Majeruhi watatu kati ya 32 waliokuwa wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam wamefariki dunia.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Stephen Kebwe amesema majeruhi hao wamefariki jana jioni Jumatano Agosti 14, 2019 hivyo kufanya idadi ya waliofariki kufikia 85.

Mkuu huyo wa mkoa amesema majeruhi 16 waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro wanaendelea vyema huku akiwaomba ndugu kujitokeza kuwajulia hali majeruhi hao pamoja na wale waliopo Muhimbili.