Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminieli Aligaesha amesema Majeruhi 6 kati ya 38 wa ajali ya moto ya mkoani Morogoro ambao walikuwa wakitibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wamefariki Dunia usiku wa kuamkia leo hospitalini hapo.

Aminiel amesema Majeruhi waliobaki ni 32 ambapo kati yao Wagonjwa 17 Wako ICU huku wengine 15 wakiwa Wodi ya Kawaida.


Kwa takwimu hizi mpya zilizotolewa leo, Mpaka sasa idadi ya waliofariki kwenye ajali hiyo itakuwa imefikia watu 82.