Wananchi wamejitokeza kwa katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Morogoro karibu kabisa na chumba cha kihifadhia maiti cha hospitali ya mkoa, ambapo zoezi la kutambua na kuaga miili ya waliofariki kwa ajali linafanyika.
Ajali hiyo ilitokea jana Jumamosi Agosti 10, 2019 katika kijiji cha Itigi, Msamvu mkoani Morogoro baada ya lori la mafuta kupinduka na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta.