Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenister Mhagama amesema Serikali imeunda kamati ya wataalamu itakayotambua maiti na majeruhi waliotokana na ajali ya lori la mafuta lililopinduka leo Jumamosi mkoani Morogoro na kulipuka.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la ajali leo, Waziri Mhagama amesema baadhi ya mawaziri watakuwa na vikao mkoani humo kujadili jinsi ya kumaliza msiba huo.


Amesema Kuna timu ambayo imeshaanza kufanya ‘assessment’ ya namna ya kuhifadhi waliofariki kwa namna yoyote ile ili ambao hawatatambuliwa serikali ya Mkoa wa Morogoro ione nini cha kufanya..


Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mjini, Mary Chonjo amesema kuanzia kesho Jumapili saa 2 asubuhi watanza kutambua miili na kuwataka wananchi waliojitokeza kutambua ndugu zao kutawanyika.