Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema karibu watu 57 wamepoteza maisha baada ya lori la mafuta ya petroli kupinduka eneo la Msamvu mkoani Morogoro na kuwaka moto

Ajali hiyo imetokea leo Jumamosi August 10, 2019 umbali wa mita 200 kutoka kituo kikuu cha mabasi Msamvu ukitokea Dar es Salaam.
Imeelezwa kuwa , baada ya lori hilo kupinduka, watu walianza kujazana wakigombania kuchota mafuta ambapo mmoja wa waliokuwa wakichota mafuta hayo alianza kuvuta betri ya gari na ikawa ndo chanzo cha moto kulipuka