Msanii wa Bongo Fleva na Diwani wa kata ya Mwanga Kaskazini, Manispaa ya Kigoma Ujiji, Revokatus Kipando maarufu kwa jina la Baba Levo amehukumiwa kifungo cha miezi mitano kwa kosa la kumshambulia Askari wa Usalama Barabarani Mkoani Kigoma.

Inadaiwa kuwa Baba Levo alimshambulia askari anayefahamika kwa jina la Msafiri Ponera, akiwa eneo lake la kazi eneo la Kwabela baada ya mtuhumiwa kulazimisha kupita kwa pikipiki wakati askari huyo akiwaruhusu watembea kwa miguu, na baada ya hapo Baba Levo aliamua kumshambulia askari huyo.