Wanamgambo wa Boko Haram, wamewaua waombolezaji 23 katika jimbo linalokumbwa na machafuko la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Wakaazi wamesema kuwa wanamgambo hao waliwashambulia waombolezaji waliohudhuria matanga katika eneo hilo.
Kiongozi mmoja wa kundi la wanamgambo Bunu Bukar Mustapha, ameeleza kuwa washambulizi waliokuwa kwenye pikipiki waliwafyatulia risasi kundi la wanaume waliokuwa wakitembea wakitoka kwenye matanga wilaya ya Ngazai karibu na mji wa Maidiguri.
Mustapha ameliambia shirika la habari la AFP kuwa walipata miili 23 kwenye eneo la mkasa huo uliotokea jana Jumamosi.
Afisa wa wilaya ya Nganzai amethibitisha mkasa huo pamoja na idadi ya waliouawa.