Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda amesema anasikia kuna mtu anatapatapa kutaka urais kwa tiketi ya CCM, kusisitiza kuwa kwa muundo wa chama hicho tawala ulivyo, jambo hilo haliwezekani.’
Pinda amesema kuwa watu wasiumize kichwa katika hilo maana amefanya kazi na marais wote waliopita na anaujua utaratibu wa chama ulivyo, hivyo Mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli anatakiwa aachwe achape kazi kwani kibaya chajiuza na kibaya chajitembeza.

“Siku zote tunaambiwa chema chajiuza na kibaya kinajitembeza, sasa huyu bwana huyu mpende msimpende ni chema kinachojiuza.

“Kwamba 2020 kuna mtu anajitokeza wala msihangaishe kichwa, msihangaishe vichwa kwenye eneo hilo ana miaka mitano na ana miaka mingine mitano, mimi nimefanya na baba wa Taifa miaka 8, mzee mwinyi 10, Mkapa 10 kwa nafasi mbili na Kikwete miaka 10.
“Kwahiyo na mimi nimo nikisema anamaliza miaka yake 10 nina uhakika na sitashangaa akimaliza miaka 10 mkasema mzee huyu angendelea.” Amesema Mizengo Pinda