Rais Magufuli ametengua uteuzi wa January Makamba ambaye alikuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira

Nafasi hiyo kwa sasa Kapewa George Simbachawene. Kupitia Ukurasa wake wa Twitter, Makamba kaweka picha yake akiwa na mzee Mwinyi na kuandika ; Kwa kweli nimeyapokea mabadiliko yaliyofanywa kwa moyo mweupe kabisa kabisa 😊. Nitasema zaidi siku zijazo.