Mbunge Nape Nnauye amesema wanaodhani kuwa wanaweza kumkwamisha Rais John Magufuli kugombea urais mwakani wanapoteza muda wao.

Nape ambaye alikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM amesema kuwa ni utaratibu wa chama hicho kuwa mtu akishapitishwa kugombea awamu ya kwanza, basi ni wazi kuwa atapitishwa kugombea awamu ya pili, na wala jambo hilo halina mjadala.
Amesema kuwa kuna makundi mawali ndani ya chama hicho yanayozungumzia suala la urais 2020. Amesema kundi la kwanzi ni la wageni (wahamiaji au wasiofahamu taratibu) ambao wanadhani kuwa Rais anaweza akazuiwa kugombea awamu ya pili.
Amesema kundi la pili ni lile la wanaofahamu taratibu za chama lakini wameamua kuwa wanafiki kuzungumzia jambo hilo.
Akizungumzia sauti zinazodaiwa kuwa ni yake akizungumza na Abdulrahman Kinana, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, amesema kuwa jambo hilo lina ujinai ndani yake hivyo, liachwe kwa vyombo husika.
Hapa chini ni mahojoano aliyoyafanya Nape kuzungumzia mambo hayo: