Shule ya Sekondari ya Nyamunga ya mkoani Mara imeshika namba moja kati ya shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2018.
Matokeo hayo yametangazwa leo Alhamisi Julai 11, 2019 na katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde.
Katika orodha hiyo kuna shule nne za Mjini Magharibi visiwani Zanzibar ambazo ni Kiembesamaki A Islamic, Mpendae, Tumekuja na Haile Selassie.
==>>Hizi ni Shule 10 za Mwisho Kitaifa
1. Nyamunga, Mara.

2. Haile Salassie Mjini Maghari.

3. Tumekuja,mjini Magharib

4. Bumaangi,mara

5. Butuli,mara

6. Mpendae, Mjini Magharib

7. Eckernford, Tanga.

8. Msimbo, Katavi.

9. Mondo, Dodoma.

10. Kiembe Samaki A Mjini Magharib