Mjukuu wa Baba wa Taifa, Mwl. JK Nyerere, Sophia Nyerere amesema haoni sura ya Babu yake kwenye sanamu iliyochongwa na kukabidhiwa kwa Rais Magufuli hivi karibuni katika uzinduzi wa Hifadhi mpya ya Burigi, Chato.
Sophia Nyerere mezungumza hayo katika mahojiano na Kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Clouds TV.
“Kiukweli sioni sura ya Babu yangu kwenye ile sanamu, aliyechora anisamehe sina nia ya kumuharibia biashara, Babu ameshafariki hawezi kujizungumzia ila tuliobaki tunatakiwa tuwazungumzie, nilisema ni mapema sana Watanzania kumsahau Baba wa Taifa.
“Nikiwa mdogo nyumbani walikuja wazungu walimletea zawadi ya sanamu nakumbuka Babu aliikataa, haikuwa moja tu zilikuwa nyingi, kuna siku ililetwa sanamu aliniambia naionaje nikamwambia huyu ni wewe ile sanamu ipo kule nyumbani Butiama” Amesema Mjukuu wa Nyerere