Kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu na wenzake watatu imeahirishwa baada ya mbunge huyo kuendelea na matibabu nje ya nchi.
Mbali na Lissu washtakiwa wengine ni Mhariri wa Gazeti la Mawio Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi..
Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde amedai mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Juni 24,2019 kuwa shauri lilikuja kwa ya kutajwa na aliomba ipangwe tarehe nyingine.
Baada ya maelezo hayo Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema washtakiwa wote wataendelea na dhamana yao na shauri hilo limeahirishwa hadi Julai 24, 2019 kwa ajili ya kutajwa.