Polisi mkoani Kilimanjaro wamekamata ndoo 60 za samaki wanaodaiwa kuvuliwa kinyume cha sheria katika Bwawa la Nyumba ya Mungu wilayani Mwanga wakiwa wanafirishwa kwenda Arusha.

Samaki hao wamekamatwa leo Juni 18 majira saa tisa usiku katika kata ya Lag’ata wilayani Mwanga ambapo Kamanda wa polisi wa Mkoa huo, Hamis Issah, amewambia wandishi wa habari kuwa samaki hao walikamatwa wakiwa kwenye aina ya Mistubishi pajero yenye namba za usajili T. 527 AEQ na kwamba wanawashikilia watuhumiwa wawili waliokutwa na samaki hao.

Amewataja watuhumiwa hao ni mfanyabishara Godlisen Mfinanga (37), mkazi Mrombo Arusha na Mwidini Seleman (30) mkazi wa kisongo Arusha na kwamba watafikishwa Mahakamani.