RAIS John Magufuli amekutana na kuzungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dkt. Josephat Gwajima leo Juni 3, 2019, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kumaliza mazungumzo yao, Gwajima amempongeza Magufuli kwa ujenzi wa mradi wa Stiegler’s Gorge akisema umeme wa mradi huo utakuwa mkubwa kuliko umeme wowote ambao Tanzania ilishawahi kuzalisha tangu uhuru, hivyo yatakuwa ni manufaa makubwa kwa taifa letu.

“Tuelewe ili ule chips yai lazima uvunje mayai, namshukuru rais kwa juhudi za Stiegler’s Gorge, tutakapozalisha umeme mwingi kuliko tuliozalisha zamani. Kama unavyojua watu wengi wa Magharibi wanasema eneo hilo ni la mazingira lakini ukweli ni siasa tu.