Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May ametangaza kuwa atajiuzulu Juni 7, 2019, baada ya kuliongoza taifa hilo kwa miaka 3.

Kiongozi huyo ambaye ni mwanamke wa pili kushika wadhifa huo amekuwa akikumbana na upinzani mkali kuhusu makubaliano ya kujitoa ndani ya Umoja wa Ulaya (EU).
Katika taarifa iliojaa hisia alioitoa huko Downing Street, Bi May amesema amefanya “kila awezalo” kutekeleza matokeo ya kura ya maoni kuhusu EU ya mnamo 2016.

Amesema ni jambo linalosalia kuwa “na majuto mengi” kwamba ameshindwa kutimiza Brexit – Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya


Bi May amesema ataendelea kuhudumu kama waziri mkuu wakati kukitarajiwa kuidhinishwa mchakato wa kumchagua kiongozi mpya wa chama cha Conservative.

Atajiuzulu kama kiongozi wa chama hicho Juni 7 na uteuzi wa waziri mkuu mpya unatarajiwa kuanza wiki inayoafuata baada ya hatua hiyo.