Mbunge wa Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi (Chadema) maarufu Sugu ameitaka Serikali kupunguza tozo kwenye Hotel kwani zimekuwa zikiwarudisha nyuma wafanyabiashara.

Mbilinyi ametoa kauli hiyo leo Mei 24 bungeni wakati akichangia Mjadala wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka 2019-2020.

Mbilinyi amesema tozo zinazotozwa kwenye hotel nchini zimekuwa nyingi hivyo ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii iziondoe ili wafanyabishara wenye biashara zao ziweze kukuwa.

“Kuhusu Tozo zimekuwa nyingi, umekaa tu mara wanapiga hodi anasema anatoka sehemu fulani,amefuata tozo, hotel mpya mzipe miaka miwili bila tozo ili wakuze biashara zao.Niiombe Serikali itoe hizo tozo zimejaa sana ndio maana biashara hazikuwi,”amesema Mbilinyi.