Kadhi Mkuu wa Tanzania, Abdallah Mnyasi amesema mfungo mtukufu wa ramadhani utaanza kesho Jumanne ya Mei 7, 2019.

Akizungumza jana Jumapili Mei 5,2019 kupitia televisheni ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wakati akifafanua kuhusu mwandamo wa mwezi alisema haujaonekana.
Alisema Waislamu kote nchini wataanza mfungo wa ramadhani mara baada ya kukamilika siku 30 za mwezi Shaaban.
Naye Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amesema kwa kushirikiana na Mufti wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaabi,na wa Tanzania Bara, Abubakar Zuber wamekubaliana mwezi haujaonekana.
Advertisements