Rais Magufuli amesema haelewi sababu za bodi za mishahara nchini Tanzania kutokutana kwa maelezo kwani yeye hana tatizo na kuonya vikao vyao kutokuwa uchochoro wa kutumia fedha za Serikali vibaya.

Ameyasema hayo leo katika sikukuu ya wafanyakazi Mei mosi, maadhimisho hayo kwa Tanzania yamefanyika katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

“Kwangu mimi hata wakitaka kukutana leo sina shida, sina tatizo namuagiza waziri mwenye dhamana kuhakikisha bodi hizo zinakutana lakini vikao vyao visiwe vichochoro vya kutumia fedha za Serikali vibaya,” amesema Rais Magufuli na kuongeza:

“Lazima nitoe angalizo hilo maana unaweza kusikia wameenda kufanya vikao Dubai lakini suala la kukutana na kujadili masuala mbalimbali kati ya wafanyakazi na yale yanayopaswa kutatuliwa mapema nasema kwa dhati sina tatizo mkutane.”

Advertisements