Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema Serikali itaendelea kulinda uhuru wa kuabudu kwa mujibu wa Katiba huku akiwapongeza Watanzania namna wanavyotumia uhuru huo bila kuuvunja.

Pia ameahidi kuwa Serikali itandelea kushirikiana na dini pamoja na madhehebu yote kwa sababu ni taasisi nyeti na muhimu katika jamii kwa sababu zinasaidia kuwafanya wananchi kuwa raia wema.

Ameyasema hayo jana Aprili 28, 2019 katika misa ya kumsimika Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga wa kanisa katoliki Jimbo Kuu la Mbeya iliyofanyika katika viwanja vya Sokoine na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Alisema amefurahi kuona katika misa ya kumsimika askofu Nyaisonga kuhudhuriwa na viongozi kutoka madhehebu mbalimbali huku akiamini pia wahudhuriaji ni kutoka sehemu tofauti.

Advertisements