Bunge limepitisha Azimio la kumzuia Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema kuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge kwa kosa la kulidhalilisha Bunge kwa kusema “Bunge ni dhaifu” na alipoitwa kwenye kamati ya Bunge ya kinga haki na madaraka ya Bunge hakuonyesha kujutia kufanya kosa hilo

Akiwasilisha hoja hiyo Bungeni leo April 4, 2019 mwenyekiti wa kamati hiyo Emmanuel Mwakasaka amesema kuwa Mbunge huyo alipopewa nafasi ya kujitetea kwenye kamati alisema ahukumiwe tu kwani alichozungumza ni kweli.
Wakati azimio hilo linapitishwa wabunge wa Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA wamesusia kikao hicho cha bunge na kutoka nje.