Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amefariki dunia leo nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu ya figo.
Ruge atakumbukwa zaidi kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya muziki nchini.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Magufuli ametoa salamu za pole kwa ndugu na jamaa kwa kuandika maneno yafuatayo: Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha kijana wangu Ruge Mutahaba. Daima nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa ktk tasnia ya habari, burudani, na juhudi za kujenga fikra za maendeleo kwa vijana. Poleni wanafamilia,ndugu,jamaa na marafiki. Mungu amweke mahali pema, Amina.


Advertisements