Wimbo mpya wa msanii Rayvanny na Diamond Platnumz ‘Tetema’ unazidi kufanya vizuri mara baada ya video ya wimbo huo kutoka.

Video ya wimbo huo imeweza kufikisha watazamaji (views) Milioni 1 kwenye mtandao wa YouTube ndani ya saa 17 pekee.
Hata hivyo Rayvanny ameshindwa kuifikia rekodi ya Diamond kupitia wimbo wake ‘Hallelujah’ aliowashirikisha Morgan Heritage ambao ulifikisha watazamaji Milioni 1 ndani ya saa 15 pekee.
Utakumbuka September 2016 video ya wimbo, Salome ambao Diamond alifanya na Rayvanny uliweza kufikisha watazamaji Milioni 1 ndani ya siku mbili pekee rekodi ambayo ilikuja kuvunjwa na wimbo wa Alikiba ambao ulifikisha idadi hiyo ya watazamaji kwa saa saa 37.

==>>Itazame hapo chini

Advertisements