Rais Magufuli amewahakikishia Watanzania wote kuwa Taifa linakwenda katika mwelekeo mzuri hasa baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha uchumi na huduma za kijamii kama vile afya, elimu, maji, nishati na miundombinu ya usafiri.

Rais Magufuli amesema hayo jana alipokutana na wananchi katika Mtaa wa Zanaki, Wilaya ya Ilala muda mfupi baada ya kutembelea Kampuni ya Africa Media Group (AMGL) yenye vituo vinne vya televisheni ikiwemo Channel Ten na vituo viwili vya redio ikiwemo Magic FM, ambayo kwa sasa inamilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Rais Magufuli amesema pamoja na mafanikio hayo, Serikali itaendelea kupambana na dhuluma na matumizi mabaya ya rasilimali za Taifa na ametoa wito kwa Watanzania wote kuiunga mkono kwa kuhakikishia wanatanguliza maslahi ya Taifa.

Advertisements