Serikali imetoa ufafanuzi kuhusu madai ya watu wa kada mbalimbali, akiwemo mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali kuwa korosho inanunuliwa chini ya Sh3,300 kinyume na agizo lililotolewa na Rais John Magufuli.

Naibu waziri wa Kilimo, Omar Mgumba ametoa ufafanuzi kuhusu bei ya korosho leo February 4, 2019 akibainisha kuwa korosho inanunuliwa kwa Sh3,300 kwa kilo moja, kwamba maagizo ya Rais hayajakiukwa.
Mgumba amesema kiasi cha Sh3,300 kwa korosho daraja la kwanza, daraja la pili ndio hununuliwa kwa Sh2,640.
Mgumba alikuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Ndanda (Chadema), Cecil Mwambe aliyetaka kujua kwa nini wanunuzi wa korosho wamekiuka agizo la Rais Magufuli na kuanza kulipa chini ya kiwango ambacho hakikuelekezwa.
==>>Tazama hapo chini

Advertisements