Msanii wa muziki kutoka WCB, Harmonize amejibu tuhuma iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwamba huwenda akawa anatumia bangi baada ya kuonekana akivuta sigara yenye moshi mzito katika moja ya video ambayo aliiweka mitandaoni.
Mkuu huyo aliyasema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na wasanii katika mkutano wa kusikiliza changamoto za wasanii na kuzitatua ambapo alizungumzia suala la nidhamu kwa wasanii hao.
Baada ya kauli hiyo, Harmonize ambaye yupo nchini Afrika Kusini amejibu tuhuma hizo kwa njia ya matani huku akilihusisha na suala la Simba kufungwa goli 5 na Al Alhy ya Misri.
Harmonizi alipost video ambayo inamuonyesha mtu akilia na kuandika; “Wakati mwingine tuacheni utani tuweni serious …!!! hivi mie niliejipost na mimoshi ya Sigara tena Sigara Embasy Hiyo Bange yenyewe naisikia kwenye Bomba…!!! na hawa wachezaji wa @simbasctanzaniaNani wakusokomezwa ndani tukitua Bongo…???? 🤣🤣🤣 hebu angalieni wanavotesa watu wasiokuwa na hatia 😭
Minazani tungeanza na @hajismanaraKwanza akamatwe achunguzwe….!!! 🤣🤣🤣🙏🙏”
Advertisements