Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetengua zuio la gawio la fedha kwa TFF ambalo lilidumu kwa takribani miaka mitatu.

Hayo yalibainishwa jana February 2, 2019 katika hotuba ya Rais wa TFF Wallace Karia kwenye Mkutano Mkuu wa TFF 2019
Kwa sasa TFF inatarajia mgao wake wa fedha za miradi mbalimbali kutoka FIFA.
“Kutokana na usimamizi wa rasirimali fedha kuimarishwa na kutekeleza mambo mbalimbali ya msingi, FIFA wamekubali kulipatia fedha shirikisho letu kama ilivyokuwa hapo awali.
“Baada ya kuimarisha usimamizi na kuwasilisha hesabu zilizokuwa zinahitajika FIFA kama ulivyokuwa utaratibu na matakwa mengine yote ya kiuhasibu, kuanzia mwaka huu tumeingia katika mpango wa kupewa fedha na FIFA kama nchi nyingine tofauti na ilivyokuwa awali.
“Fedha ambazo tulikuwa hatujazipokea nazo tutazipata. Shirikisho bado linachukua hatua thabiti kwenye usimamizi wa rasilimali fedha kwa kudhibiti matumizi yasiyokuwa ya lazima, kuhakiki madeni kabla ya malipo na kufanya malipo kwa njia ya ki-electronic.”-Alisema Karia
Advertisements