Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemjulia Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Utakumbuka January 31 mwaka huu Spika wa Bunge Job Ndugai aliagana na Mbunge huyo katika Uwanja wa Ndege wa Jijini Dodoma kabla ya kusafirishwa kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.