Mtoto wa miaka 10, ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili, amekutwa ameuawa kikatili na mwili wake kutelekezwa kichakani eneo la Lupembe, wilayani Njombe wakati akitoka shuleni jana.

Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema:,” Ni kweli mtoto kwa jina Rachael Malekela (7), mwanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Matembewe ameuawa nyuma tu ya nyumba yao na kutupwa kwenye shamba la miti.”

Mwenyekiti wa kijiji cha Matembwe, Brayson Malekela amesema wazazi wa mtoto huyo walibaini kutoonekana nyumbani jana saa 12 jioni, walitoa taarifa katika uongozi wa kijiji na wananchi kuanza kumtafuta na saa 4 usiku walikuta mwili wa mtoto huyo katika msitu wa miti mipana uliopo kijijini hapo.

Advertisements