Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametangaza vita kali kwa viongozi wa kisiasa wenye tabia ya kuwatusi na kuwadhalilisha kwa namna yoyote viongozi wa dini kuwa atawakamata na kuwachukulia hatua kali za kisheria.
RC Makonda ameonyesha kusikitishwa na tabia iliyoibuka ya baadhi ya wanasiasa wanaowatolea maneno yasiyokuwa na heshima Viongozi wa Dini jambo ambalo ameeleza kuwa hawezi kuvumilia kuliona katika Mkoa anaoongoza.
Aidha RC Makonda amesema Viongozi wa Dini wamekuwa na mchango mkubwa katika jamii hivyo wanapaswa kuheshimiwa na sio kudhalilishwa na wachache wasiokuwa na maadili.
Makonda ameyasema hayo jana wakati wa ufunguzi wa majengo mapya ya Bweni la wasichana, Ukumbi na gari ya shule ya Sekondari St. Joseph Millennium ya Goba.
Advertisements