Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa TBC, Tido Mhando, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.
Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya upande wa mashtaka kushindwa kudhibitisha mashtaka yake.

Tido alifikishwa Kisutu kwa mara ya kwanza Januari 26, 2018, kujibu mashtaka matano.

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 7/2018, Tido alikabiliwa na mashtaka matano, mashtaka manne ni ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887.1 milioni.

Advertisements