Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabohora Tanzania, Zainuddin Adamjeeameshangazwa na tabia ya vyombo vya habari kufanya matangazo ya michezo ya kubahatisha licha ya kuwa ni haramu katika dini zote.
Adamjee akizungumza leo katika kikao kati ya Rais John Magufuli na viongozi wa madhehebu ya dini Ikulu jijini Dar es Salaam.

“Kwenye Biblia na Quran imeandikwa kamari ni haramu, lakini hapa TZ saivi Vijana wanacheza kamari kupitia Mitandao ukifungua TV unakuta matangazo, haya Makampuni wao ni hapa kamari tu, matatizo nguvu kazi yetu inacheza kamari.”Amesema

Amesema wakati Taifa likiangalia matatizo yako wapi asitafutwe mchawi kwa sababu shida ni kuwa nguvu kazi inacheza kamari.