Msanii wa Muziki kutoka lebo ya WCB, Rayvanny ameeleza vile anavyojisikia baada ya kufunguliwa na Baraza la Sanaa la Taifa-BASATA.

Rayvanny na Diamond Walifungiwa kujihusisha na sanaa kwa muda usiojulikana baada ya kutoa Wimbo wa Mwanza, ambao haukuwa na maudhui mazuri.
Rayvanny ameiambia Wasafi Tv amelishukuru Baraza, Wizara na Serikali na wale wote waliokuwa wanatamani wao wafunguliwe.
“Kiukweli unapopata habari nzuri lazima ufurahi, kiukweli nimefurahi sana, kwasababu nilikuwa kwenye situation ambayo ni sintofahamu kiukweli then hivi vitu ndio first time kuviface hivi vitu, niseme tu nashukuru serikali, nashukuru Baraza, Wizara pia nawashukuru na wale waliokuwa wanatamani sisi kufunguliwa,” amesema Rayvanny.
Msikilize Hapo chini

Advertisements