Rais wa Tanzania, John Magufuli ameshindwa kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika leo Jumamosi Januari 12, 2019 katika Uwanja wa Gombani, Pemba visiwani humo.

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein akihutubia mamia ya wananchi na viongozi mbalimbali waliojitokeza uwanja hapo amesema Rais Magufuli amesema hajaudhuria sherehe hizo kwa sababu amepata dharura.

Viongozi wengine waliohudhuria ni; Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, marais wastaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi na Jakaya Kikwete.

Advertisements