Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa

ILIPOISHIA
Gari nne nyeusi, zenye muundo wa gari kama zinazo bebea pesa za mabenki, zikafunga breki katika eneo tulilopo. Wakashuka watu walio valia ñguo nyeusi, makofia meusi yaliyo waficha sura zao, na kubakishs macho yao tu. Kila mmoja mkononi mwake ameshika bundiki, na wote wakanizungu huku wakinitazama kwa umakini.
ENDELEA
Mmmoja wao akatoa amri ya mimi kuiamsha mikono yangu juu, nikatii pasipo kubishana. Akatoa amri nyingine ya mimi kulala chini, hapo ndipo nilipo anza kuleta ubishi, kwani siwezi kukamatika kirahisi.
Kitendo cha mimi kusogeza mguu nyuma, nikastukia kitu chenye ncha kali kikinichoma mgongoni, kwa haraka nikaupeleka mkono wangu nyuma, kwa ajili ya kukichomoa. Nikakuta ni sindano
yenye dawa, iliyo anza kuvinyong’onyeza viungo vyangu vya mwili. Taratibunikajikuta nikianza kuishiwa na nguvu. Nikaanguka chini, kila nilipo jaribu kunyanyua hata mkono sikuweza, nikajikuta nikiwatazama watu hao walio nikaribia na kuninyanyua. Nikastukia kitu kizito kikinipiga, kichwani, giza kali likanitawala machoni mwangu.
********
“Eddy…. Eddy”
Nisauti nyororo, iliyo anza kuisikia taratibu, ikipenya masikioni mwangu. Taratibu nikayafungua macho yangi, nikakutana na sura ya kike, huku kichwa chache kikiwa kimejaa nywele nyingi nyeusi na zilizo ndefu sana.
Macho yake makubwa kiasi, na yadura kiasi, yaliendelea kunitazama huku akiwa ameniimamia, kutoka katika kitanda nilicho kilala.
“Karibu tena duniani” Alizungumza huku akiwa ametabasamu.
“Duniani?”
“Ndio duniani”
“Kwani nilikua, sipo duniani?”
Hakuzungumza chochote zaidi ya kusimama, pembeni ya kitanda nilicho lala.
“Kwa jina ninaitwa dokta, Agines, nimtaalamu katika maswala ya saikolojia”
“Ngoja, hapa ni wapi?”
“Upo Washinton DC, Marekani”
“Ahaaaa?”
“Usishangae, ninaimani kwamna unatambua, nitukio gani ulilo lifanya kwa ajili ya hii nchi, nasi tumeamua kukuweka karibu nasi na kukusaidia kwa kila jambo”
Akafungua pazia, kubwa lililopo kwenye moja ya ukuta, hapa ndipo nilipo anza kuona majengo makubwa yaliyopo katika mji huu, ambapo ndipo yalipo makao makuu ya serikali ya nchi ya Marekani.
“Tutahakikisha tunakufanyia kila unacho kihitaji”
Akaniandalia chakula, akaniomba nile.
“Ukimaliza kula, kuna watu nitahitaji uonane nao”
“Wakina nani?”
“Utawaona tuu”
Nikamaliza kula, akanionyesha bafuni, nikaoga na kurudi kitandani, huku nikiwa nimejifunga taulo.
“Unaweza kuvaa”
“Mbele yako?”
“Kwani kuna tatizo lolote, tambua kwamba mimi nitakuwa pamoja nawe kwakipindi cha siku tisini”
“Za nini?”
“Eddy vaa bwana, watu hao wanakusubiri.”
Nikamtazama kwa muda, nikavua taulo, nikachukua nguo moja baada ya nyingine alizo zipanga kwenye kitanda.
“Umependeza sana”
“Asante”
“Upo tayari”
“Ndio”
Tukatoka ndani ya chumba, hichi kilicho tengenezwa kwa mfumo wa wakisasa, tukaingia ndani ya lifti na kushuka chini, hapa ndipo nilipo gundua ghorofa tuliyokuwa ni ya hamsini kutoka chini.
Tukafika chini, kabisa tukaongozana hadi nje ya ghorofa hili, tukakuta gari karibia sita zenye muundo mmoja wa milango sita zikitusubiri sisi.
Tukaingia kwenye moja ya gari, na gari zote zikaondoka.
“Tunapo kwenda ni wapi?”
“Ahaaa utapaona usiwe na wasiwasi”
Akanipa glasi iliyo jaa whyne
“Ninaamini unatunia hiki kinywaji?”
“Ndio”
Nikaendelea kutazama jinsi mji huu ulivyo jengeka, kwa majengo marefu. Tukafika kwenye mojo ya geti kubwa, gari zote zikaingia kwa pamoja.
Tukashuka mimi na Agie, tukapokelewa na mdada mmoja aliye valia suti nyeusi. Akatupeleka kwenye moja ya meli, iliyo simama pembezoni mwa bahari
“Ni nani huyo tunakwenda kuonana naye?”
“Eddy mbona una haraka, utamuona tu”
Tukaingia ndani kabisa ya meli hii ya kifahari, kila niliye mtazama alionekana kutabasamu. Wengine wakadiriki kunisalimia, kwafuraha.
“Tuingue humu chumbani”
Tukaingia kwenye moja ya chumba kilicho humu ndani ya meli hii. Tukakuta baadi ya watu wanao onekana ni wanamitindo.
Wakanichukua vipimo vya mwili wangu, wakaanza kunishonea nguo ya mtindo nilio uchangua kati ya mitindo mingi, waliyo nionyesha.
“Agie mbona, mimi sielewi?”
“Huelewi nini Eddy?”
“Mambo yote haya, munanifanyia kwa maana ipi?”
“Eddy kama nilivyo kuambia, inatupasa kulufanyia kitu kama kukulipa fadhila ya uliyo fanya kwa raia wa Marekani”
“Hata kama, ila bado haijaniingia akilini!”
“Kwa nini?”
“Ni watu wangapi, walikufa kwa ajili ya wamarekani muliwafanyia hivi?”
“Ndio ila kila mmoja ana bahati na nafasi yake kwenye maisha. Kwahiyo nafasi yako no hii”
Ndani ya lisaa, nguo niliyo hitaji kushonewa ikawa imekamilika, wakanipa niijaribu, kutokana na uzoefu wao, hawakukosea kitu hata kimoja.
“Ni muda wakutoka kwenda kukutana na watu nilio, kuahidi utaonana nao”
Nikashusha pumzi huku nikimtazama Agie, ambaye naye, alibadilisha nguo alizo kuja nazo na kuvalia gauni, refu jekundu.
Tukatoka tukiwa tumeshikana mikono, sauti yakiume, kupitia kipaza sauti nikaisikia ililitaja jina langu, ukumbi wote ukafura kelele za makofi. Watu walizidi kushangilia huku wakianza kuimba wimbo wa Happy birtday, wakiashiria ni siku yàngu ya kuzaliwa.
Agie akanipeleka hadi mbele ya ukumvi kwenye sehemu iliyo nyanyuka kidogo. Kwa matatizo yalivyo nizonga, hata siku yangu ya kuzaliwa sikuikumbuka.
Ukimya ukatawala ndani ya ukumbi, huku watu wakinisubiri nizungumze kitu chochote.
“Kipindi, nilipo kuzaa, nilitambua kwamba ipo siku utakuja kua mtu muhimu kati ya watu wengi ulimwenguni humu”
Sauti ya mama, ilinistua, kupitia vipaza sauti vilivyomo humu ndani, nikatazama pande zote za ukumvi ila sikumuona mama.
“Usipate shida ya kunitafuta, nipo hapa mwanangu”
Nikamuona mama, akisimama katikati ya watu huku mkononi mwake akiwa ameshika kipaza sauti.
“Leo maombi yàngu, Mungu ameyasikia. Nilikutafuta kwa miaka mingi mwanangu. Hadi leo nimekuona”
Mama alizungumza huku akipiga hatua akija mbele nilipo, mashafu ya mama yakaanza kujaa machozi, yanayo mtiririka kutoka machoni mwake.
“Umekua mwanangu, hadi leo unatimiza miaka ishirini na tato, kweli umekua mwanangu”
Nikashikwa na kigugumizi hata sikuweza kuzungumza, mama akanikaribia na kunitazama usoni mwangu, nami nikashindwa kuyazuia machozi yangu. Tukajikuta tukikumbatiana kwa pamoja na kuwafanya watu, waliopo ukumbini kupiga makofi
“Nakupenda sana mwanangu, Eddy”
Sikutarajia kama ninaweza kukutana na mama yangu, baye nimepotezana naye kwa kipindi kirefu sana
“NA…KU..PENDA PIA MAMA”
Nilizungumza huku, machozi yakinimwagika, yakiendana na sauti iliyo jaa kigugumizi. Kati ya watu walio simama ukumbibi, nikamuona Sheila, akipiga makofi huku akimwagikwa na machozi ya furaha
SORRY MADAM 80
Taratibu mama akaniachia na kunibusu kwenye paji la uso wangu. Akasimama pembeni yangu nakuniomba nizungumze chochote, kwa watu walio nifanya sasa hivi kuwa na furaha.
“Siamini, kitu ninacho kiona mbele ya macho yangu.”
Nilizungumza huku nikijifuta machozi yafuraha yanayo nimwagika usoni mwangu.
“Sina kitu kingine chakuzungumza zaidi ya kusema asanteni, nyinyi nyote. Mulio nikutanisha na familia yangu. Asanteni sana.”
Nikamapa kipaza sauti, muendeshaji wa shughuli hii, mama akaninishika mkono na kunipeleka kwenye moja ya meza, iliyo na kitu kikubwa kilicho funikwa na kitambaa cheupe.
“Eddy tunakuomba ufunue hicho kitambaa”
Muongozaji wa shughuli alizungumza nami nikafanya kama alivyo zungumza. Sikuamini kuona keki kubwa, iliyo tengenezwa kwa muonekano wangu.
Nguo zilizo tengenezwa kwenye, keki hii, ni zile nilizo kua nimezivaa siku nilivyo kua katika mapambano, ya kumuokoa balozi wa marekani na familia yake, huku mkononi nikiwa nimeshika bastola. Wadada wawili walio valia sare nzuri za suti zenye rangi ya ‘cream’ wakasimama karibu yangu na kuanza kuikata kekii hii, yenye maandishi yaliyo andikwa kwenye kibao cheusi ambacho nacho pia ni keki, yanayo someka
(Wewe nishujaa wa maisha yangu na familia yangu, hongera kwa siku yako ya kuzaliwa)
Wakamaliza kukata vioande vya keki, kisha muongoza sherehe akaniomba nianze kumlisha mtu nimpendaye. Nikamuanza mama, kisha nikamuita balozi Brayan, pamoja na familia yake. Nafasi yangu ya mwisho nikamuita Sheila, ambaye katika, ziku alizo pendeza ni leo. Ukumbi wote ukakaa kimya, kusikilizia ni kitu gani ninaweza kukifanya, baada ya Sheila kusimama mbe yangu, akisubiria mimi nimlishe keki. Nikachukua moja ya kipande, nikakiweka mdomoni mwangu, kisha taratibu, nikakipeleka mdomoni mwa Sheila, watu wote waliopo ukumbini, wakatusindikiza kwa kupiga makofi.
“Nakupenda mume wangu”
Sheila lizungumza, huku machozi yakiendelea kumbubujika usoni mwake.
“Ninakupenda pia, mke wangu”
Tumaendelea, kunyonyana midomo yetu mbele ya mama, pamoja na watu wote walio hudhuria sherehe yangu ya kuzaliwa.
Mziki wa taratibu ukafunguliwa, kila mtu aliye na mpenzi wake, hakusita kumshika alipo jisikia, nakucheza taratibu. Nikaanza kucheza na Sheila baada ya muda, nikabadilishana na mzee mmoja aliyekuwa akicheza na mama, akahamia kwangu
“Eheee Eddy mwanangu umekua, mbaba, hadi nakushangaa”
“Kwa nini mama?”
“Mara ya mwisho kukuacha ulikuwa kijana mdogo”
“Ndio hivyo mama”
“Ehee ulikua wapi kipindi chote, nilikutafuta hadi nikakata tamaa na kujua kwamba umefariki?”
“Usijali mama, nitakuadisia, ila vipi baba?”
“Yule shetani!”
Kwa jinsi mama, alivyo zungumza alinifanya, nitabasamu, kwani alionekana kukerwa sana na mzes Godwin
“Ndio, huyo huyo Shetani”
“likamatwa, nakufungwa”
“Amefungwa wapi?”
“Ahaa Embu achanana na hizo habari mwanangu, tuendelee kusherekea”
“Sawa, je kazini umerudi?”
“Ndio nimerudi kitambo sana, sasa hivi mimi ni waziri mkuu”
“Kweli mama?”
“Ndio mwanangu, ila kunakitu kimoja nahitaji ukitekeleze hivi karibuni”
“Kitu gani mama?”
“Nahitaji uniletee mkwe, na sihitaji mwanamke mwengine isipo kua Sheila”
“Sawa mama”
“Usiseme sawa, nahitaji pia na mjukuu wa kucheza naye, nina miaka hamsini sasa, hata kuitwa bibi, sijaitwa bado”
“Ila mama, mi..”
Nikajikuta nikinyamaza gafla, sikutaka kumuambia mama, kama nina mtoto, nimezaa na Phidaya, ila kitu kunacho nifanya nisizungumze, ni kuto kumuoba mwanangu.
“Ila nini?”
“Mtoto ni najaliwa ya Mungu”
Nilibadilisha mada haraka, ili mama asielewe nini kinacho endelea moyoni moyoni mwangu.
“Ndio hapo muombe, kwa Mungu awajalie, mumpate”
“Unataka wa kike au wakiume?”
“Mimi yoyote, ili mradi awe mjukuu wangu”
Mama akarudi kwa mzee mwenzake, nami nikarudi kwa Sheila, tukaendelea kuburudika ma miziki inayo badilika badilka kila wakati.
Tukaongozana na Sheila hadi eneo la juu la Meli hii, hapa ndipo nikagundua kwamba meli, inatembea, kwani sehemu tuliyopo sasa, ni katikati ya bahari na magorofa yote sikuyaona, zaidi ya jua linalo zama kwa mbali, nakutengeneza rangi nzuri kama nyekundu kwenye, mawingu.
Tulibaki kutazamana na Sheila, pasipo kuzungumza kitu cha aina yoyote, kila mmoja, anatafakari kitu cha kuzumgumza kwa wakati huu.
“Eddy”
Sheila aliniita kwa sauti ya chini na yaupole.
“Mmm”
“Ninakupenda”
“Ninakupenda pia”
“Kweli?”
“Ndio”
Kwa haraka, Sheila akaniparamia, mwilini mwake, huku mikono yake akiipitisha, shingoni mwangu na kuikutanish nyuma yangu, tukaanza kunyonyana midomo yetu, huku kila mmoja akitoa nihemo ya mahaba. Kila mmoja ana hamu na mwenzake, jambo liito tukuta tukianza kupapasana kila kona ya mwili, huku mikono yangu nikiipeleka kwenye makalio ya Sheila, yaliyo makubwa kiasi na malaini.
“Eddy stop, stop”
“Nini?”
“Hii sehemu si sahihi, twende huku”
Sheila akanishika mkono na kushuka ngazi, tukaelekea sehemu yenye vyumba, akafungua moja ya chumba, tukaingia ndani. Macho yangu yakanza kukishangaa hichi chumba kwani kwenye madirisha yake mawili, unaona samaki walio chini ya maji.
“Unashanga nini?”
“Hichi chumba kipo chini ehee?”
“Ndio, kipo kwa ajili yetu,”
Sheila alizunfumza huku akifungua mikanda ya viatu vyake virefu, Sheila akanifwata na kunikumbatia, huku akiendelea kuninyonya mdomo wangu.
Kwa jinsi mahaba, yalivyo tuchanganya, sote tukaangukia kitandani, na kuendea kutomasana, kila kona ya mwili, huku tukisaidiana, kuvuana nguo, tukabaki kama tulivyo zaliwa, na tukazama kwenye dimbwi zito la mahaba.
******
Safari ya kufika kwenye bandari ya Mombasa, nchini Kenya, ilitugharimu siku kumi na sita, usiku na mchana, kupiti meli hii ya kifahari, yenye huduma za kila aina. Katika kipindi chote cha safari, niliweza kukutana na watu maarufu, wengine nikaingia nao mikataba ya matangazo kwenye makampuni yao mbalimbali, ikiwemo kampuni ta magari aina ya Ford.
Kwa mikataba niliyo ipata, imeaniingizia kiasi cha pesa zaidi ya milioni thelathini za dola ya kimarekani. Pia ndani ya meli, niliweza kutengeneza matangazo mawili, moja likiwa la mafuta ya nywele kwa ajili ya wanaume, na jengine lilikua ni kwaajili ya kuchangia wahanga wa ugonjwa wa Ebola.
Tukapanda ndege ya kukodi, hadi uwanja wa CIA uliopo mkoani Arusha. Mama akatangulia Dar es Salam, akatuacha mimi na Sheila, nikimalizia kufanya baadhi ya matangazo niliyo ingia mikataba. Na mengine yalisha anzs kurushwa kwenye baadhi ya vituo vikubwa duniani, kama BBC, SKYSPORT, BEINGSPORT na vinginvyo.
“Mume wangu kuna simu yako inaita”
Sheila alizungumza huku, akiwa ameishika simu yangu. Tukiwa kwenye moja ya eneo tulilo panga kumalizia, kipande cha mwisho cha utengenezaji wa video, ya tangazo kwa ajili ya magari ya kampuni ya Ford
“Nani?”
“Namba mpya, sijui ya nchi gani?”
Nikachukua simu yangu na kuipokea na kuiweka sikioni kusikiliza ni nani anaye piga
“Eddy mimi ni Casey, nimeona tangazo lako yaani, kaka umejitahidi”
“Asante mdogo wangu, mbona tena namba mpa upo wapi?”
“Nimerudi Canada kusoma, namalizia muhula wa mwisho”
“Ahaa sawa, asante”
“Nilimaliza tuu kaka, kabla sijakwenda Afrika kusini, nitakuja Tanzania nikae kae na wifi”
“Usijali mdogo wangu, baadaye kidogo kuna kazi naifanya watu wananisubiria mimi tu”
“Ahaa sawa kaka yangu, ngoja nikuache baadaye”
“Sawa”
Nikakata simu na kumrudishia Sheila, mimi nikaingia kwenye gari ninalo fanyia tangazo.
“Baby simu yako inaita tena”
“Nani?”
“Namba ngeni?”
“Pokea muambie, ninakazi nafanya”
Nikaendelea kufwata maelekezo, ninayo pewa na muongozaji wa tangazo, nikimuacha Sheila akiendelea na kuzungumza na simu.
Nikafanikiwa kumaliza, tangazo hili, lililo kua gumu, kidogo kwangu kulifanya. Tukatlrudishwa kwenye hoteli tuliyo fikizia, na dereva wa kampuni hii ya Ford. Tukaingia kwenye chumba chetu, huku nikiwa nimechoka kiasi
“Eddy mama ameniambia tarehe ya harusi, waliyo panga kwenye kikao?”
“Tarehe ngapi?”
“Kumi”
“Ahaa si wiki mbili zimesalia”
“Ndio”
“Wameiharakisha, sana”
“Kwani tatizo lipo wapi, kwanza hapa nina habari njema kwetu”
“Habari gani?”
“Sijaziona siku zangu, nahisi nimenasa tayari”
“Ina maana una mimba yangu!”
“Ndio mume wangu, mimba ni yako, kwani hakuna mwengine zaidi yako aliye nigusa mimi”
Nikamfwata Sheila na kumkumbatia kwa furaha, huku nikimzungusha zungusha hewani na kumsimamisha chini, huku nikimbusu busu mdomoni mwake”
“Ngoja kwanza, baby nahitaji unijibu swali langu?”
“Uliza tu mke wangu nitakujibu haraka haraka”
Nilizungumza kwa furaha, kwa huku nikilisubiria kwa hamu swali ka mke wangu mtarajiwa Sheila
“PHIDAYA NI NANI YAKO?”
“Eheeee!”
“Hujanisikia nirudie au?”
Sheila alizumgumza, huku akinitazama kwa sura iliyo anza kujikunja kwa hasira kali.
==> ITAENDELEA

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia mbukuzi blog

Advertisements