Kijana anayedaiwa kuzaa na msichana wa kazi aliyedai mwanaye wa miezi mitano alikuwa akifungiwa kabatini na mwajiri wake tangu alipozaliwa, amekamatwa na polisi mkoani Dodoma.

Kijana huyo, Salum Waziri, amekamatwa baada ya agizo lililotolewa na mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi.
Katambi alisema Waziri amekamatwa kwa tuhuma za kumpa ujauzito Neema Matimbe ambaye ana miaka 15, ambaye alikuwa mfanyakazi wa ndani wa mwalimu, Anitha Kimako.
Alisema pamoja na tuhuma zinazomkabili Anitha kuwa alimfungia kabatini mtoto wa binti huyo, kulikuwa na ulazima wa kumsaka kwanza baba mzazi wa mtoto yuko kwa sababu alifanya kitendo hicho kwa binti mwenye umri chini ya miaka 18.
Katambi alisema kijana huyo ni mkazi wa Area C alikataa mimba ya mtoto huyo.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa, William Mkonda alisema kijana huyo atafikishwa mahakamani muda wowote uchunguzi utakapokamilika.
Advertisements