Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ameeleza kuwa wamepanga kwenda mahakamani kuhusu sakata la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Prof. Mussa Assad.

“Baada ya kushauriana na Wanasheria na Wabunge tumeona ni muhimu sana kwa maslahi mapana ya nchi yetu kulinda Katiba yetu. Baadhi ya Wabunge kutoka vyama vyote tumeamua kwenda mahakamani kuomba tafsiri ya KINGA ya CAG kwa mujibu wa Katiba na mamlaka ya Spika kutoa Wito kwa CAG,”ameandsika Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Utakumbuka hapo jana Spika Ndugai alimtaka CAG, Prof. Mussa Assad kufika mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Januari 21 mwaka huu kujieleza kufuatia kauli za kudhalilisha Bunge